India yaamriwa kufutilia mbali leseni

Mahakama ya juu nchini India imeamuru serikali ifutilie mbali leseni za kampuni za simu za mkononi zilizotolewa kwa kampuni za mawasiliano miaka minne iliyopita.

Sakata hiyo ndiyo kubwa zaidi ya ufisadi kuwahi kutokea nchini India.

Mhasibu wa umma nchi humo amesema sakata hiyo imeigharimu wizara ya fedha mabilioni ya dola.

Waziri aliyehusika na uuzaji wa leseni hizo anakabiliwa na kesi ambapo anashtumiwa kwa kupokea hongo.

Hata hivyo amekanusha madai hayo.

Waandishi wa habari wanasema sakata hiyo imesababisha ghadhabu nchini India.