Argentina kushtaki Uingereza kwa UN

Rais wa Argentina, Cristina de Kichner, amesema taifa lake litawasilisha rasmi malalamiko yake kwa Umoja wa Mataifa kwa kile ambacho amesema ni kuimarishwa kwa wanajeshi wa Uingereza katika eneo la Kusini mwa Bahari ya Atlantic.

Uingereza imewatuma wanajeshi katika visiwa vya Falkland vinavyozozaniwa kati ya Argentina na Uingereza.

Akitoa hotuba, Bi Kichner amesema ni jambo la kusikitisha kuwa katika karne hii ya 21 mataifa mengine yangali yakikusudia kuendelea kuwa na makoloni.

Alishutumu hatua ya Uingereza ya kutuma meli ya kijeshi hadi Kusini mwa Bahari ya Atlantic. Bi Kirchner amesema hatua hiyo itaweza kuchukuliwa tu kama kuimarisha majeshi eneo hilo.