Boko Haram yakiri kutekeleza shambulio

Wapiganaji wa Kiislam wa kundi lenye itikadi kali la Boko Haram wamekiri kwamba walifanya shambulio la kujilipua nje ya kambi ya jeshi katika jiji la Kaduna nchini Nigeria.

Mtu mmoja aliyevaa nguo za kijeshi alijilipua nje ya kambi hiyo ambayo ni mojawapo wa kambi ambazo zina ulinzi mkali nchini humo.

Msemaji wa kundi la Boko Haram pia amesema kwamba walijaribu kutekeleza shambulio lingine katika kambi ya askari wa anga.

Kundi hilo limesema linataka kupindua serikali ya Nigeria na badala yake kuhakikisha nchi hiyo inatawaliwa kwa mujibu wa sheria za kiislamu.

Wanamgambo wa Kiislam wameua mamia ya watu kaskazini mwa Nigeria.