Vikwazo vya silaha Sudan havitekelezwi

Shirika la kimataifa la Haki za Kibinadamu la Amnesty limetoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuimarisha na kutilia mkazo zaidi vikwazo vya silaha dhidi ya Jamhuri ya Sudan.

Amnesty ilisema kuwa hatua ya dharura inapaswa kuchukuliwa upesi kufuatia ushahidi unaoonyesha kuwa silaha kutoka Uchina, Urusi na Belarus zinaendelea kutumiwa kuwaua raia kutoka maeneo ya Darfur, kinyume cha vikwazo vya silaha vilivyowekewa taifa hilo mwaka 2004.

Hofu kubwa ya silaha hizo ni kuwa zinatumika katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Umoja wa mataifa unakadiria kuwa kuna zaidi ya watu 300,000 wamekufa kwa karibu kipindi cha miaka kumi wakati machafuko kwenye eneo la Darfur yalianza ingawaje serikali inasema ni watu elfu kumi pekee wamefariki.