Pakistan:Mahakama yafuta rufaa ya Gilani

Mahakama kuu nchini Pakistan imetupilia mbali rufaa ya waziri mkuu wa nchi hiyo dhidi ya mashitaka yanayomkabili ya kudharau mahakama hiyo.

Ina maana kuwa Bwana Yusuf Raza Gilani atatakiwa kufika mbele ya mahakama kuu wiki ijayo kusikiliza mashitaka dhidi yake ya kukataa kuchunguza tuhuma za ufisadi zinazomkabili rais wa nchi hiyo.

Waziri mkuu hakuwa mahakamani leo, lakini wakili wake amesema Yusuf Raza Gilani hakudharau mahakama kwa kukataa kuchunguza madai ya ufisadi dhidi ya rais.

Wakili huyo wa waziri mkuu, amesema Rais Asif Ali Zardari, akiwa mkuu wa nchi, sheria zinamlinda kutoshitakiwa.