Kifo cha Whitney: hakuna "mkono wa mtu"

Afisa wa uchunguzi mjini Los Angeles, Marekani amesema hakuna dalili za kuwepo na uhalifu katika kifo cha mwimbaji Whitney Houston.

Baada ya kufanya uchunguzi, mtaalam huyo alisema hakuna dalili zozote zinazoonekana kwenye mwili wa Houston na hakuna wasiwasi wa kuwepo na "mkono wa mtu" kwa sasa.

Amesema maafisa bado wanachunguza, lakini hadi wapate matokeo ya uchunguzi mwingine, wataendelea kutazama sababu nyinginezo.

Msanii huyo alikutwa amekufa bafuni katika hoteli moja mjini Los Angeles, siku ya Jumamosi.