Imam mashuhuri mahakamani Kenya

Imam mmoja mashuhuri nchini Kenya, Aboud Rogo, anayetuhumiwa kuwa mlezi wa kundi la Al-shabaab nchini Kenya, amefikishwa mahakamani katika mji wa Mombasa .

Rogo amefunguliwa mashtaka ya kumiliki silaha hatari kinyume cha sheria, kupanga njama ya kutekeleza mauaji na kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi la Al-shabaab.

Polisi walimkamata Sheikh Aboud Rogo nyumbani kwake akiwa na silaha hatari zikiwemo bunduki, guruneti na vilipua mabomu.