Vurugu zatokea jela Nigeria

Shambulio dhidi ya gereza moja nchini Nigeria, limepelekea kuachiwa huru kwa wafungwa miambili. Mlinzi mmoja wa gereza hilo aliuawa wakati watu waliokuwa wamejihami walivamia gereza hilo, katika mji ulioko kusini mwa mji mkuu Abuja.

Mfungwa mmoja anaaminika aliachwa nyuma. Msemaji wa idara ya magereza alikanusha kuwa kundi la Boko Haram lilihusika na shambulio hilo.

Hata hivyo alikataa kuelezea kwa nini alikanusha kuhusika kwa Boko Haram. Mwezi Septemba mwaka 2010, kundi la Boko Haram lilifanikiwa kuhusika katika kusaidia wafungwa mia saba kutoroka katika tukio sawia na hilo.