Libya:Mwaka 1baada ya Gaddafi kuondolewa

Imebadilishwa: 17 Februari, 2012 - Saa 08:27 GMT

Wananchi wa Libya wanaadhimisha mwaka mmoja tangu kuanza kwa harakati za kumuondoa mamlakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi.

Sherehe zimepangwa kufanyika katika miji kote nchini humo.

Vituo vya ukaguzi vimewekwa ili kuzuia sherehe hizo kutatizwa.

Mkaazi mmoja wa Benghazi ameiambia BBC kuwa hawezi kuamini mabadiliko yaliyotokea nchini Libya katika kipindi cha mwaka mmoja.

Machafuko yameongezeka nchini humo katika siku za hivi karibuni huku serikali ikijaribu kukabiliana na wapiganaji wenye silaha ambao walisaidia katika harakati za kumuondoa Kanali Gaddafi.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.