Riek Machar azungumzia mzozo wa mafuta

Makamu wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar ameiambia BBC kuwa nchi yake itaendelea, licha ya kusitisha uzalishaji wa mafuta kufuatia mzozo kati yake na Sudan.

Ushuru unaotokana na mafuta huchangia asilimia 98 ya mapato ya serikali.

Bwana Machar amesema Sudan Kusini italazimika kusimamisha maendeleo kwa muda wa miaka michache.

Hata hivyo amesisitiza huduma za msingi hazitaathirika, ikiwemo mishahara ya wafanyikazi wa serikali na jeshi.