Vikwazo kuendelea Zimbabwe

Shirika la kutetea haki za binadamu Human, Rights Watch limetaka Jumuiya ya Ulaya kuendelea na vikwazo vya usafiri dhidi ya kiongozi wa Zimbabwe Robert Mugabe sawa na kushikilia mali yake na ile ya wanachama katika chama talawa.

Human Rights watch inasema wanaharakati wa kidemokrasia wanaendelea kuhangaishwa na serikali na haikuona haja ya kuondoa vikwazo dhidi ya baadhi ya viongozi wakuu serikalini.

Kumekuwa na taarifa kwamba Jumuiya ya Ulaya inanuia kuviondoa vikwazo vilivyowekewa baadhi ya viongozi wa serikali nchini Zimbabwe pamoja na maafisa wa chama tawala kwanzia leo.