Utafiti waonya kuhusu chumvi baharini

Utafiti mpya unaonyesha kuwa iwapo hali ya chumvi itaongezeka katika bahari duniani basi asilimia 30 ya viumbe wa bahari watafariki kufikia mwishoni mwa karne hii.

Kiwango cha chumvi huongezeka kutokana na gesi ya carbon dioxide na wanasayansi katika chuo kikuu cha Plymouth nchini Uingereza wanachunguza volkeno chini ya bahari kuona iwapo viumbe wa bahari watamudu hali hiyo katika siku za usoni.

Wanasema katika kipindi cha miaka michache ijayo athari hiyo inaweza kuanza kudhihirika.