Kesi ya raia wa Uingereza yaahirishwa

Kesi ya raia wa Uingereza anayeshutumiwa kwa madai ya kupanga shambulio la bomu ilianza leo nchini Kenya kabla ya kuahirishwa hadi mwezi Mei.

Jermaine Grant kutoka mashariki mwa London alitiwa mbaroni kwa pamoja na washukiwa wengine watatu mwezi Disemba.

Kesi hiyo iliahirishwa kuruhusu ushahidi fulani kuchunguzwa zaidi nchini Uingereza.

Polisi wa Kenya wanadai Grant ana uhusiano na wapiganaji wa Al- shabaab nchini Somalia.