Kesi dhidi ya Bradley Manning imeanza

Kesi inayomkabili mwanajeshi mmoja wa Marekani, Bradley Manning, imeanza.

Bradley amefunguliwa mashtaka kwa kutoa maelfu ya nyaraka muhimu kisiri kwa mtandao wa Wikileaks.

Manning, mwenye cheo cha Private, ambaye hadi sasa amekana tuhuma hizo anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha jela ikiwa atapatikana na hatia. Mshukiwa huyo anakabiliwa na mashtaka 22 likiwemo shtaka la kusaidia adui.

Mwandishi wa BBC mjini Washington, anasema wafuasi wa Private Manning, wanamuangalia kama shujaa kwa kujitolea kupata adhabu kali kutoa mwanga kuhusu jinsi Marekani inavyoendesha vita, lakini wakosoaji wake wanamuangalia kama msaliti ambaye hajali usalama wa nchi yake.