Uchaguzi kufanyika Jumapili, Senegal

Waziri mkuu wa senegal , Souleymane Ndene N'Diaye, anasema uchaguzi mkuu utafayika nchini humo kama ulivyopangwa siku ya Jumapili.

Baadhi ya makundi ya upinzani yametoa wito uchaguzi huo uahirishwe na kuapa kuwa nchi hiyo haitakuwa na uongozi ikiwa Abdoulaye Wade mwenye umri wa miaka 85 atakataa kuanchia madaraka .

Wade anawania muhula wa tatu kuwa rais wa nchi hiyo, licha ya kwamba katiba ya sasa ya haimruhusu kufanya hivyo .

Rais wa zamani wa Nigeria , Olusegun Obasanjo, anakutana na viongozi wa upinzani akiwemo mwanamuziki Youssou N'Dour, kujaribu kutuliza mvutano wa kisiasa.

Youssou N'Dour amekatazwa kugombea wadhifa huo wa urais.