Uchaguzi wa ubunge wafanyika Iran

Vituo vya kupigia kura vimefungwa Iran katika uchaguzi wa wabunge baada ya kuongezwa muda wa saa tano kutokana na watu wengi kujitokeza kupiga kura, vyombo vya habari vya serikali vimesema.

Ni uchaguzi wa kwanza tangu kuwe na maandamano yaliyochochewa na ushindi wenye utata wa Mahmoud mwaka 2009.

Shughuli ya Upigaji kura inafanyika nchiniIrankatika Uchaguzi wa kwanza wa Kitaifa tokea ufanyike Uchaguzi wa URAIS ulioleta Mabishano miaka mitatu iliyoopita ambao Rais Ahmedi-Nejad alishinda.

Uchaguzi huu wa sasa ni wa bunge la taifa, na ushindani mkali baina ya makundi mawili yenye itikadi kali yaliyo karibu sana na kiongozi wa kidini Ayatollah Ali Khamenei na wafuasi wa rais Ahmadi Nejad.

Upande wa Upinzani umeusussia Uchaguzi huu, huku Wakuu wake wengi wakiwa wamekataliwa Kugombea au wamepewa Kifungo cha Nyumbani.