Moto baharini Nigeria hatimaye wazima

Moto uliozuka na kuteketeza mtambo wa kuchimba gesi kwenye ufuo wa bahari nchini Nigeria, na kusababisha vifo vya watu wawili, hatimaye umezimika baada ya siku arobaini na sita.

Kampuni inayoendesha shughuli ya uchimbaji ya Chevron, ilisema kuwa moto ulizima bila usaidizi wowote.

Wanaharakati wa shirika la Friends of the Earth wanaitaka kampuni hiyo kuwalipa fidia wavuvi wa Nigeria kwa kupoteza pato lao wakati moto ulipozuka.