Internet kudhibitiwa zaidi nchini Iran

Kiongozi wa kidini nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameamuru kuundwa kwa jopo maalum litakalosimamia matumizi ya internet nchini humo.

Tangazo hilo lililotolewa kwenye vyombo vya habari vya serikali, lilielezea kuwa jopo hilo litajumuisha rais, mawaziri wa mawasiliano na utamaduni, polisi na makamanda wa jeshi la nchi.

Hii inaaminika kuwa hatua kali zaidi kuchukuliwa hivi karibuni na watawala wa Iran katika kudhibiti matumizi ya Internet.