Baraza la mpito kuilinda Libya

Kiongozi wa baraza la kitaifa la mpito nchini Libya, Mustafa Abdel Jalil, amesema yuko tayari kutetea umoja wa nchi hiyo kwa nguvu.

Bwana Abdel Jalil, alitoa matamshi hayo siku moja baada ya viongozi wa kikoo pamoja na makamanda wa wapiganaji mashariki mwa Libya kutangaza kujitawala.

Aidha Abdel Jalil amewataka viongozi wa eneo hilo kushiriki kwenye mjadala. Amelaumu pendekezo hilo kwa wale wanaotaka kuzua tu vurugu akiongeza kuwa ni watu waliokuwa wafuasi wa utawala wa Muamar Gadafi.

Lakini alisema serikali ya kitaifa haiko tayari kuigawanya Libya.