Hali ya wanaharakati yazorota China

Kundi moja maarufu la kutetea haki za binadamu nchini Uchina limesema kuwa hali ya wanaharakati nchini humo imezidi kuwa mbaya zaidi.

Hii ni katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita huku zaidi ya wanaharati alfu nne wa kisiasa wakizuiliwa.

Kundi hilo lenye makaazi yake katika mji wa Hong Kong- kwa jina Chinese Human Rights Defenders, linasema kuwa maafisa wa serikali wameimarisha udhalimu wao dhidi ya wapinzani.

Wanasema ni kufuatia wito wa kuanzishwa kwa vuguvugu la mapinduzi nchini humo kama yaliyoshuhudiwa katika mashariki ya kati.

Kundi hilo linasema zaidi ya wanaharakati mia moja hamsini kati ya wale waliozuiliwa waliteswa.

Beijing imesisitiza kuwa taifa hilo linaongozwa na mfumo wa sheria.