Afghanistan yaelezea kukerwa na mauaji

Bunge la Afghanistan limepitisha azimio la kushutumu kitendo cha mwanajeshi wa Marekani aliyewaua raia 16 wa Afghanistan.

Bunge hilo lilisema Afghanistan imechoshwa na vitendo vya wanajeshi wa kigeni nchini Afghanistan na likasema kuwa mwanajeshi huyo lazima afunguliwe mashtaka nchini Afghanistan.

Awali Rais wa taifa hilo alituma ujumbe maalumu kwenda hadi Kandahar kuchunguza mauaji hayo.

Miongoni mwa watu waliouawa wakati wa tukio hilo siku ya Jumamosi ni watoto tisa

Rais Obama ameomba msamaha kwa niaba ya Marekani na kueleza masikitiko yake kuhusiana na mauaji hayo. Lakini mwandishi wa BBC mjini Kabul anasema uhusiano kati ya mataifa hayo mawili tayari umeharibika.