Ataka kuuawa kutokana na maumivu

Muingereza ambaye mwili wake mzima umepooza sana kiasi cha kutaka dakatari amuue amepewa idhini apeleke kesi yake katika Mahakama Kuu ya nchi hiyo.

Tony Nicklison, mwenye umri wa miaka 58, anataka daktari yeyote anayekubali maombi yake asikabiliwe na mashtaka ya mauaji.

Wizara ya Haki ya Uingereza inapinga ombi hilo la Bwana Nicklison. Bwana Nicklson alipooza mwaka 2005 na wakati huu anakabiliwa na maradhi yajulikanayo kama "locked in syndrome" ambapo mwili wake umepooza lakini akili yake ni timamu.

Mwandishi wa BBC wa maswala ya kisheria anasema kesi hiyo itajadili maswala yanayozidi mtu kusaidiwa kujiua, kwa sababu Bwana Nicklson anataka mtu wa kumwua sio wa kumsaidia kujiua kwa sababu hana uwezo huo.