Makabiliano mapya Sudan kusini

Mamia ya watu hawajulikani waliko wengi wao wakihofiwa kufariki kufuatia makabiliano mapya Sudan Kusini.

Wapiganaji waliokuwa wamejihami kwa silaha nzito nzito kutoka kabila la Murle waliiba maelfu ya mifugo wakati wa uvamizi katika maeneo kadhaa katika jimbo la Jonglei.

Afisaa mmoja wa serikali alifahamisha BBC kuwa takriban watu miambili walijeruhiwa wakati wa mashambulizi katika eneo la Akobo mnamo siku ya Ijumaa.

Ghasia zilizosababishwa na wizi wa mifugo pamoja na mapigano ya kulipiza kisasi kati ya makabila ya Murle na Luo Nuer yamewaacha maelfu ya watu wameuawa tangu Sudan kusini kupata uhuru wake.