Ajali ya basi Switzerland

Takriban watu 28 wakiwemo watoto 22 wamekufa kwenye ajali ya basi iliyotokea katika Barbara ya chini kwa chini nchini Switzerland.

Wengine 24 walijeruhiwa katika ajali hiyo karibu na Sierre, katika mji wa Valais, ulio mpakani na Italia.

Basi hilo lilikuwa limewabeba abiria 52 kuelekea Ubelgiji baada ya michezo ya kutereza kwenye barafu. Inasemekana liligonga ukuta wa njia hiyo ya chini kwa chini siku ya Jumanne.

Waziri mkuu wa Ubelgiji, Elio Di Rupo alisema 'ni siku ya huzuni kubwa kwa Ubelgiji yote.'

Mjini Brussels, na waziri wa mambo ya nje wa Ubelgiji alisema wengi wa watoto hao walikuwa na umri wa miaka 12. Basi hiyo ilikuwa mojawapo ya magari yaliyokodiwa na kundi la Kikristo kuwasafirisha watoto hao kwa michezo. Mengine mawili yalifika salama.