Waziri wa Marekani azuru Afghanistan

Waziri wa ulinzi wa Marekani Leon Panetta, ameanza ziara ya ghafla nchini Afghanistan.

Panetta aliwasili nchini humo katika kambi moja ya kijeshi ya Bastion kusini mwa mkoa wa Helmand, kwa mazungumzo na makamanda wa jeshi la Marekani nchini humo na maafisa wa serikali ya nchi hiyo.

Pannetta vile vile anatarajiwa kufanya mazungumzo na rais wa nchi hiyo Hamid Karzai.

Panneta anawasili nchini humo huku kukiwa na gadhabu nyingi nchini humo kufuatia mauaji ya raia kumi na sita yaliyotekelezwa na mwanajeshi wa marekani siku ya jumapili.

Inadaiwa kuwa mwanajeshi huyo aliwaua raia hao ambao walikuwa katika nyumba kadhaa katika eneo la Panjwayi mkoani Kandahakar.