Taliban lasitisha mazungumzo na Marekani

Kundi la Taliban nchini Afghanistan limesitisha mazungumzo yake ya Marekani kuhusu kufungua ofisi hya kisiasa nchini Qatar na mpango wa ubadilishanaji wa wafungwa.

Ripoti zinasema Marekani ilitaka serikali ya Afghanistan kushiriki katika mazungumzo hayo, pendekezo ambalo limepingwa vikali na kundi hilo la Taleban.

Hii ni kwa kwa sababu kundi hilo halitambui utawala wa rais Hamid Karzai .

Chini ya mpango wa ubadilishanaji wa wafungwa, wapiganaji watano wa Taleban ambao wanazuiliwa na wanajeshi wa kimataifa wangelikabithiwa kwa kundi hilo na badala yake kundi hilo kumuachilia huru mwanajeshi mmoja wa Marekani ambaye anazuiliwa na kundi hilo.

Katika tukio lingine rais Karzai ameagiza wanajeshi wa NATO kurejea katika kambi zao kufuatia kuuawa kwa raia kumi na sita mwishoni mwa juma lililopita.