Boko Haram yapinga mazungumzo

Msemaji wa kundi la kiisilamu la Boko Haram nchini Nigeria amesema hawatafanya mazungumzo yeyote na serikali. Msemaji huyo amewaambia waandishi wa habari kuwa hawana tena imani na serikali.

Mapema mwakani rais GoodLuck Johnathan alitaka kundi hilo la Boko Haram kuanza mazungumzo kama njia ya kumaliza machafuko ambayo yamesababisha vifo vya mamia ya watu.

Kundi la Boko Haramu ambalo liliundwa miaka kumi iliyopita limetekeleza mashambulio kadhaa yakilenga maafisa wa usalama, makanisa pamoja na afisi ya Umoja wa Mataifa mjini Abuja.

Kundi hilo limesisitiza kwamba serikali haijatekeleza masharti yao ya kuwaachiwa huru wanachama wake wanaozuiliwa na maafisa wa usalama.