Burma yawaalika waangalizi wa kimataifa

Serikali ya burma imewaalika waangalizi wa uchuguzi kutoka marekani na jumuia ya ulaya kuchunguza uchaguzi ujao.

Viti arobaini na vinane vinagombaniwa katika uchaguzi huo wa mwezi aprili.

Kwa mara ya kwanza kiongozi wa upinzani na mshindi wa tuzo ya nobel Aung San Suu Kyi atawania kiti kimoja cha ubunge.

Hiyo jumanne jumuia ya mataifa ya kusini na mashariki mwa asia ASEAN ilisema kuwa imeruhusiwa kupelea waangalizi 23 nchini humo.