Mashambulio ya jeshi Damascus

Wanaharakati wa upinzani nchini Syria wamesema jeshi la serikali limeshambulia kwa makombora maeneo mawili yaliyoko mji mkuu Damascus.

Mashambulizi hayo yalianza baada ya wapiganaji kulenga afisi ya ujasusi.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameonya dunia dhidi ya kupuuza mzozo unaoendelea nchini Syria.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kukutana baadaye leo mjini New York kujaribu kuafikiana mpango wa amani ambao umependekezwa na mjumbe wake Koffi Annan.

Taarifa hiyo haitakuwa inaufunga upande wowote na halitakuwa azimio rasmi la baraza hilo.