Iran yadaiwa kusaidia Sudan kwa silaha

Maafisa wa Sudan Kusini wamelaumu utawala wa Iran kwa kutoa makombora kwa jirani wake Jamuhuri ya Sudan.

Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini amesema ndege iliyodunguliwa katika jimbo la Kordofan Kusini ilipatikana na mabomu yaliyowekwa alama ya Iran.

Sudan Kusini pia imelaumu Sudan kwa kuendelea kuwasajili wapiganaji wa kijamii katika eneo la mpaka kama jaribio la kujitayarisha kwa mashambulizi.

Serikali ya Sudan imeomba jeshi la kikabila maarufu kama Popular Militia kama hatua ya kuzima maasi ya kundi moja lililoshirikiana na waasi wa SPLA ambao walipata uhuru wa Sudan Kusini Julai mwaka jana.