Hussein Salem kurejeshwa Misri

Duru za kisheria nchini Misri, zimefahamisha BBC kuwa Misri imekubali masharti ya Uhispania ya kumrejesha nchini humo kwa mfanyabiashara tajiri mkubwa ambaye alikuwa msaidizi wa rais aliyeng'olewa mamlakani Hosni Mubarak.

Uhispania ilimkamata Hussein Salem mwaka jana na kuibana akaunti yake yenye mamilioni ya dola pamoja na kuzuia mali yake mjini Marbella, kusini mwa Uhispania.

Duru ziinaarifu kuwa Misri imeihakikishia Uhispania kuwa itampa hukumu ya haki bwana Hussein Salem,na hivyo Uhispania kukubalia kumrjesha Misri bwana huyo.

Wananchi wengi wa Misri, wanataka wafanyabiashara waliojitajirisha kwa njia fisadi chini ya utawala wa Mubarak, kuchukuliwa hatua za kisheria.