Wapiganaji arobaini wauawa Yemen

Maafisa nchini Yemen wanasema kuwa takriban wapiganaji arobaini wameuawa katika shambulio la angani kusini mwa nchi hiyo.

Maafisa hao wamesema kuwa shambulio hilo limepiga eneo lililokumbwa na mapigano kati ya majeshi ya serikali na wapiganaji wa kiislamu yaliyokuwa yamechacha kwa siku kadhaa na kusababisha majeruhi kutoka pande zote.

Wapiganaji hao wanadaiwa kuwa wa kundi la AL qaeda japo hakujatolewa thibitisho la hilo.

Kundi lililohusishwa na Al qaeda Ansar al Sharia, limekuwa likizidisha oparesheni zake katika eneo la kusini mwa Yemen kwa mwaka mmoja uliopita na kuhujumu uthabiti wa taifa hilo .