Magendo ya sigara kuzimwa

Zaidi ya nchi 130 zimeafikiana hatua za kupambana na biashara ya magendo ya sigara katika mkutano wa shirika la afya duniani WHO mjini Geneva,Switzerland.

Mpango huo ni pamoja na mfumo mpya wa kutoa leseni na utaratibu wa kimataifa kufuatilia sigara inavyohamishwa kutoka eneo moja hadi jingine. WHO inasema kupambana na magendo kutasaidia nchi kuokoa zaidi ya dola bilioni 40 katika mapato ya kodi yanayopotea bure.