Majenerali washtakiwa Uturuki

Majenerali wawili wakongwe waliohudumu katika jeshi la Uturuki wamefikishwa mahakamani leo katika kile kinachoonekana kama kesi ya kihistoria.

Majenerali Kenan Evren na Tahsin Sahinkaya ndio viongozi pekee wangali hai waliohusika katika mapinduzi ya kijeshi yaliyoung'oa uliokuwa utawala wa Uturuki mwaka 1980.

Mamia ya waandamanaji walikusanyika nje ya mahakama wakidai haki kwa watu mia tatu na hamsini waliouawa au kufariki dunia wakati wakizuiliwa baada ya mapinduzi.

Inaarifiwa wakati wa mapinduzi hayo, Jenerali Evren alisema mauaji ya washukiwa hayapaswi kuhojiwa, akiongeza kuwa kwani walipaswa kuwalisha magaidi au kuwanyonga.