Raia wa Ufaransa wakamatwa Somaliland

Maafisa wa utawala wa Somaliland, wameelezea kuwakamata raia wawili wa Ufaransa walioingia nchini humo kinyume na sheria kutoka nchini Djibouti.

Wanne hao wameelezewa kuingia nchini humo kwa magari mawili ya kibinafsi, bila visa.

Polisi wamesema kuwa watu hao wamepelekwa mjini Hergeisa kwa uchunguzi zaidi.

Taarifa zinaarifu kuwa watu hao walipatikana na nakala za mafunzo ya kiisilamu wakati walipokamatwa.

Kumeripotiwa wasiwasi kuhusu idadi kubwa ya wafanyakazi wa kujitolea wa kigeni wanaoingia nchini Somalia kusaidia kundi la Al shabaab katika vita vyao.