Rais wa kwanza Algeria Ben Bella afariki

Rais wa kwanza wa kuchaguliwa nchini Algeria, Ahmed Ben Bella, amefariki dunia katika umri wa miaka tisini na sita.

Alikuwa mmoja wa watu walioongoza vita vya Algeria kupata uhuru kutoka kwa Mfaransa nusu karne iliyopita.

Mwaka 1962 akawa waziri mkuu wa kwanza wa Algeria mpya baadaye akapinduliwa na kufungwa miaka mitatu baadaye.

Ben Bella alikimbilia uhamishoni nchini Switzerland; na baadaye alirejea Algeria mwaka 1990 lakini hakuwa na mvuto mkubwa kisiasa.