Rais Kabila akutana na maafisa wa jeshi

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amefanya mikutano ya dharura na viongozi wa kijeshi huko Mashariki mwa nchi hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya mamia ya wanajeshi kuondoka kutoka katika kambi zao.

Inaaminiwa kuwa wanajeshi hao walioondoka ni watiifu kwa Jenerali Bosco Ntaganda.

Ntaganda aliyekuwa kiongozi wa waasi anayejulikana kama "Terminator".

Anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu. ICC , kwa mashitaka ya kuwasajili watoto katika jeshi.

Mwezi uliopita mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama hiyo ya ICC ametoa mwito wa kukamatwa Jenerali Ntaganda, baada ya mahakama ya ICC kumpata na hatia Kiongozi wa zamani wa waasi Thomas Lubanga kwa mashitaka kama hayo.