Santorum ajiondoa ugombezi wa Republican

Mmoja wa wagombea uteuzi wa urais wa Marekani kupitia chama cha Republican, Rick Santorum, amesema atajiondoa katika kinyang'anyiro hicho, akimwacha Mitt Romney kuwa mgombea kupitia chama hicho ambaye huenda akapambana na Rais Obama mwezi Novemba.

Bwana Santorum, mwenye msimamo usiopenda mabadiliko, ametoa tangazo hilo nyumbani kwake katika jimbo la Pennsylvania akiandamana na familia yake.

Alipata umaarufu kwa ushindi wa kushtukiza huko Iowa mwezi Januari lakini ameachwa nyuma na Bwana Romney mfanyabiashara tajiri.

Hakuweza kumtaja Mitt Romney kuwa anamuunga mkono katika azma ya kuwakilisha chama cha Republican.