Vikosi vya Syria kuondoka makazi ya raia

Serikali ya Syria imetangaza kuwa Jeshi lake litasimamisha harakati zake zote za kijeshi alhamisi wiki hii.

Wizara ya ulinzi ya SYRIA ilitoa tangazo lake hilo kupitia Televisheni ya Taifa.

Mjumbe wa kimataifa kuhusu Syria Koffi Annan amesema serikali ya Syria imemjulisha kuhusu uamuzi huo.

Tangazo hili linakuja wakati kumekuwa na taarifa kadhaa kutoka kwa wanaharakati katika mji wa Homms wakielezea mashambulio yanayoendelea kufanywa na vikosi vya serikali.

Picha za moja-kwa-moja za video zimekuwa zikionesha mashambulio ya Kijeshi.Mashambulizi hayo yalitakiwa kusitishwa na vikosi vya kijeshi kuondoka tangu jana jumanne.

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa mpango wa amani wa Umoja wa Mataifa Bw. Koffi Annan.