Sudan Kusini, Khartoum washauriane - AU

Muungano wa Afrika umetoa wito kwa Sudan Kusini na Jamhuri ya Sudan kurejelea mashauriano ya kuleta amani kati yao.

Hii inafuatia hatua ya Sudan Kusini kuteka eneo la Heglig, lililo na mafuta mengi, ambalo Sudan ya Khartoum inadai ni lake.

Naibu wa mwenyekiti wa Tume ya Afrika, Erustus Mwencha, ametoa wito kwa mataifa hayo kusitisha vita kati yao.

Akizungumza na BBC kwa njia ya simu, naibu mwenyekiti wa Tume ya Afrika, Erustus Mwencha, aliambia BBC kuwa ni muhimu kwa Sudan Kusini na Jamhuri ya Sudan kuendelea na mazungumzo ya amani kwa sababu ni kwa manufaa ya mataifa yote mawili.