Berlusconi alipia karamu za makahaba

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Silvio Berlusconi

Mwanamitindo wa kike ameambia mahakama mjini Milan kwamba alilipwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Silvio Berlusconi, kuwa kwenye karamu ya makahaba.

Mwanamke huyo Imane Fadil ameelezea kuwaona wanawake waliovalia kama watawa wakivua nguo zao, kubakia uchi mbele ya Bw.Berlusconi.

Waziri Mkuu huyo wa zamani amekanusha kujua ikiwa wanawake walioalikwa katika karamu zake walikuwa malaya au kufanya ngono na wasichana wa umri mdogo.

Wakati huo huo, polisi wa Italia wamemkamata mtoro Valter Lavitola, ambaye anaaminika kuwa agenti aliyewatafuta makahaba na kuwapeleka kwa Silvio Berlusconi.