Ingabire hatafika tena mahakamani

Image caption Ingabire mahakamani

Mmoja wa viongozi wa upinzani nchini Rwanda amejiondoa kutoka kesi inayomkabili ya ugaidi. Victoire Ingabire amesema hatafika wala kutuma mawakili wake mahakamani.

Ingabire ameshtakiwa kwa kutishia usalama wa nchi, kukanusha kuwepo mauaji ya Kimabari pamoja na kuchochea chuki za kikabila.

Amekuwa kizuizini tangu mwaka wa 2010 baada ya kurejea nchini Rwanda kutoka uhamishoni ambapo alitaka kushiriki uchaguzi wa urais.

Waendesha mashtaka wamesema hatua yake haina maana yeyote na kwamba kesi hiyo itaendelea bila yeye kuwepo.