Machafuko ya Syria yatishia waangalizi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waangalizi wa Syria

Marekani imeonya kwamba machafuko yanayoendelea nchini Syria yanatishia mpango wa kuwatuma waangalizi 200 wa kimataifa wanatarajiwa nchini humo.

Onyo hilo limetolewa na mjumbe wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Susan Rice wakati waangalizi sita wameanza shughuli zao mjini Damascus.

Umoja wa Mataifa unatarajiwa kuidhinisha waangalizi wote baadaye wiki hii.

Makundi ya upinzani yamesema wanajeshi wa serikali wameendelea kushambulia mji wa Homs ambapo watu 30 waliuawa.