Rufaa ya wagombea 10 Misri yatemwa nje

Shirika la habari nchini Misri limesema rufaa iliyokatwa na wagombea 10 wa urais dhidi ya kukataliwa maombi yao imetupwa nje.

Miongoni mwa wanasiasa hao ni pamoja na aliyekuwa mkuu wa ujasusi wakati wa utawala wa rais Mubarak Omar Suleiman, mgombea wa chama cha Muslim Brotherhood Khairat al-Shater pamoja na ,Hazem Salah Abu Ismail anayetetea sera kali za kiisilamu.

Uchaguzi wa urais unafanyika mwezi ujao ambao unatajwa kama hatua muhimu ya mageuzi baada ya rais Mubarak kuondolewa kufuatia mandamano ya umma.