Brotherhood yahofia demokrasia Misri

Mgombea wa Urais kutoka chama cha Muslim Brotherhood, nchini Misri ambaye amefutiwa kuwania nafasi hiyo ameonya kuwa mageuzi kuelekea demokrasia yako hatarini.

Akizungumza na BBC Khairet el-Shater amesema Muslim Brotherhood wataongeza shinikizo ndani na nje ya Bunge kuhakikish kuwa mageuzi ya kidemokraisa yanaendela na kuzuia jaribio lolote la udanganyifu katika uchaguzi.

Chama hicho tayari kinasema kinaunga mkono kuteuliwa kwa Mohamed al-Mursi, chaguo lake la pili lakini anachukuliwa kutokuwa mgombea mwenye ushawishi mkubwa.