Aung San Kyi kuzuru Norway, Uingereza

Kiongozi wa upinzani nchini Burma, Aung San Suu Kyi, anapanga kufanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi hiyo baada ya miongo miwili.

Msemaji wa upinzani alisema mwanasiasa huyo atazuru nchi za Norway na Uingereza mwezi Juni.

Bi Suu Kyi amenukuliwa majuzi akisema anapanga kufanya ziara ya nje ya nchi kufuatia mabadiliko ya kisiasa nchini mwake yaliyomuezesha kuchaguliwa mbunge kwa mara ya kwanza.

Aliishi miaka 15 kizuizini na kupuuza shinikizo za kumtaka asizuru nje ya nchi kwa hofu angezuiwa kurudi nyumbani.