Marekani yalaani picha za askari na maiti

Waziri wa ulinzi wa Marekani Leon Panetta, na Kamanda mkuu wa majeshi ya Marekani nchini Afghanistan, Jenerali John Allen, wamelaani vitendo vya wanajeshi wa Marekani kupiga picha kando ya maiti za watu waliojilipua kwa kujitoa mhanga.

Picha hizo zilichapishwa na gazeti la Marekani Los Angeles Times licha ya ushauri wa idara ya ulinzi kutozichapisha.

Jenerali Allen amesema idara ya ulinzi inafanya uchunguzi kamili.

Mapema mwaka huu Wanajeshi wa Marekani walihusika na tukio lililozua maandamano nchini Afghanistan walipoteketeza nakala za Koran.