Mauaji ya raia Iraq

Takriban watu thelathini na watano wameuawa katika mfululizo wa mashambulio ya mabomu kote nchini humo.

Katika mji mkuu Baghdad maeneo ya shia, yalilengwa zaidi. Waziri wa Afya Majeed Hamad Amin, amenusurika kuuawa katika eneo hilo wakati bomu lililotegwa garini mwake kulipuka.

Kumekuwa na mashambulio zaidi katika miji ya Kirkuk na Samarra kaskazini mwa nchi hiyo.

Mwandishi wa BBC mjini Baghdad anasema huenda mashambulio hayo ni ya kupangwa.