Mshukiwa wa genocide arejeshwa Rwanda

Kwa mara ya kwanza mahakama ya umoja wa mataifa inayosikiliza Kesi kuhusu Rwanda , huko Tanzania, imerejesha nchini Rwanda , mshukiwa wa mauaji ya kimbare ... Jean Bosco Uwi-Kindi kufunguliwa Mashtaka huko

Wakili wa mshukiwa huyo amesema mteja wake amesafirishwa kwa ndege na kurejeshwa muda mfupi tu baada ya rufaa yake kukataliwa.

Upande wa utetezi umedai kuwa bwana Uwinkindi ambaye ni kasisi wa zamani na anayeshukiwa kuongoza mauaji ya watutsi karibu na kanisa lake hatopata haki nchini Rwanda.

Maelfu ya watutsi pamoja na wahutu wenye msimamo wa kadri waliuawa kwenye mauaji ya kimbare yaliyokumba nchi hiyo mwaka 1994.