Kampeini za Urais zaanza Misri

Kampeini za urais nchini Misri zimeanza rasmi leo. Imesalia majuma matatu kabla ya taifa hilo kufanya uchaguzi mkuu wa kwanza huru.

Kumekuwepo na mzozo kabla ya kampeini hizi huku baadhi ya wagombea wakuu wakifutiwa maombi yao ya kugombea urais.

Mwandishi wa BBC mjini Cairo amesema ushindani mkali ni kati ya wagombea wawili wanaotetea sera za kiisilamu Abd-el-Mon'im Abul-Fotooh na Mohammad Morsi pia yuko aliyekuwa Mkuu wa Jumuiya ya nchi za kiarabu Amr Moussa.

Hapo Jumapili chama kikuu cha kisiasa Muslim Brotherhood, kimesema watawala wa kijeshi wameridhia mabadiliko ya baraza la mawaziri.